Monday 17 June 2013

(NEWS) DRAKE ATANGAZA KUFANYA TOUR KATIKA MAJIJI 41

     Drake atangaza tour kwa ajili ya maandalizi ya kupush album yake itakayokwenda kwa jina la Nothing was the same.
    Tour hiyo itafanyika maeneo ya Amerika ya kaskazini na atakuwa na wasanii ambao watampiga tafu katika tour hiyo ambao ni Future na Miguel. Tour hiyo itapita kwenye majiji 41 na itaanza September 25

(NEWS) ALBUM YA KANYE WEST YAVUJA MTANDAONI

      Yakiwa yamebakia masaa kadhaa album ya Kanye West kuachiwa rasmi limeibuka balaa lingine ambalo lime mchanganya Yeezy.
      Habari zinasema kuwa album hiyo inayokwenda kwa jina la Yeezus imevuja siku ya ijumaa na wataalamu wanasema ishu hiyo imemchanganya Kanye ambaye hivi sasa ni baba wa mtoto mmoja. Kampuni ya Kanye imeshaanza kushughulikia wahusika wanao husika na kuvujisha album hiyo na wamesema watawachukulia hatua za kisheria kwani wamevuruga biashara.
    Kumekua na tabia ya uvujishaji wa album za masuper star sana na taarifa zinasema kuwa watu wa karibu na ma-star ndio wamekuwa wakihusika zaidi 

(NEWS) JAY Z ATANGAZA ALBUM MPYA NA SIKU YA KUTOKA

    Akiwa ameshaingia kwenye dili na kampuni ya Samsung  Jay Z ametaja jina la album na tarehe ambayo album hiyo itatoka.
   Jay Z alifunguka na kusema kuwa album itakwenda kwa jina la "Magna Carta Holy Grail" itakuwa available kuanzia July 4 kwa wateja milioni moja wa Samsung ambao watakua wanatumia application maalumu kwaajili ya kuipata album hiyo na kwa watumiaji wengine itakuwa available baada ya masaa 72 baada ya kuachiwa  July 4 na tayari kampuni ya Samsung imeshanunua nakala zaidi ya milioni za album hiyo ya Jay Z.

Friday 14 June 2013

HAWA NDIO WASANII WA TANO WA MUSIC WENYE GARI ZA THAMANI

1:Sean Combs, a.k.a. P Diddy anamiliki gari aina ya Rolls Royce       

2:Shawn Carter, a.k.a. Jay-Z anamiliki gari aina ya Maybach Exelero

3: Andre Young, a.k.a. Dr. Dre anamiliki gari aina ya Hummer H2



4:Bryan Williams, a.k.a. Birdman anamiliki gari aina ya Lamborghini Veneno

5:Curtis Jackson, a.k.a. 50 Cent anamiliki gari aina ya Ferrari

(NEWS) JUNE 18 INASUBIRIWA KWA HAMU NA WADAU WA MUZIKI DUNIANI

         Wapenzi wengi wa muziki wakiwa wanasubiri kwa shauku kubwa album za wanamuziki maarufu Kanye West na J.Cole ambazo zote zitatoka siku moja ambayo ni June 18 kuna mastaa wengine wamekuwa na ya kuongea kuhusiana na shughuli hii nzito inayosubiriwa kuona ni nani atakae ongoza kwa mauzo ya album.
      Mac Miller ameweza kuongea kwa upande wake akisema yeye anaamini kuwa Kanye West ndiye atakae ibuka kidedea kwenye battle hiyo na kusema muziki wa Kanye ni mkubwa na kwamba si wa kupambana na bwana mdogo J Cole. Ikumbukwe kuwa J Cole amekuwa akihairisha utoaji wa album mara kibao aliamua kuirudisha nyuma kutoka tarehe 25 June mpaka 18 June ili kupambana na Kanye West.
    Album ya J.Cole inakwenda kwa jina la Born sinner ambayo inatolewa chini ya Bad Boys Rec na ya Kanye West inakwenda kwa jina la Yeezus  ambayo inatolewa na G.O.O.D Music zote zinategemewa kutoka tarehe 18 June mwaka huu.

Thursday 13 June 2013

(NEWS) MWEZI MBAYA KWA 2 CHAINZ(Tity Boi)

  Ukiwa sio mwezi mzuri kwa rapper 2 Chainz kutokana na kukumbwa na misala kila kukicha. Baada ya jana kuonekana akiwa amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Los Angels International Airport kutokana na kutuhumiwa kukutwa na bangi leo kimenuka tena.
  Akiwa maeneo ya San Fransico mkali huyu alivamiwa na wakabaji(waporaji) ambapo pia ilisikika milio ya risasi pande hizo. Inasemekana 2 Chainz alikuwa na wapambe wake lakini baada ya kusikia milio ya risasi walijikuta wa kihangaika kukimbia huku na kule kama mende. Wakabaji hao walifanikiwa kuondoka na pochi ya rapper huyo, lakini lakumshukuru Mungu rapper huyo hakuweza kujeruhiwa na risasi pia 2 Chainz alikataa kuzungumza na police kwa kusema atashughulikia tatizo mwenyewe.

(NEWS) LANGA AFARIKI DUNIA LEO SAA KUMI JIONI

  Msanii aliyekuwa akiwakilisha vizuri muziki wa BongoFleva kwa upande wa Hip Hop anaefahamika kwa jina la Langa Kileo amefariki leo jioni.
  Akidhibitisha taarifa hizo baba mzazi wa msanii huyu, anasema Langa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
  Taratibu za msiba zinaendelea nyumbani kwao Mikocheni na mama mzazi wa msanii anatarajiwa kufika nchini kesho akitokea nchini Marekani.
  Mungu ailaze roho ya marehemu Langa mahala pema peponi.

Monday 10 June 2013

(AUDIO) Ciara-Boy Outta Here


(NEWS) UTATA WA MASHAIRI ULIOPO KATIKA NYIMBO YA MILEY WAWACHANGANYA MASHABIKI

   Utata wa mashairi uliopo katika single mpya "We can't stop" ya mwanadada Miley umewafanya mashabiki wake kujiuliza  kuumiza vichwa sana kwani wameshindwa kuelewa msanii huyu ameimba nini.
  Ngoma hiyo ambayo itapatikana katika album mpya ya Miley ambayo inategemewa kutoka mwaka, mashabiki wengi wanashindwa kuelewa kuwa kwenye ngoma hiyo mwanadada ameimba "dancing with Molly" au ni "dancing with Miley".
  Akizungumzia kuhusiana na ishu hiyo producer alietengeneza ngoma hiyo Mike Will Made It amesema kuwa vyovyote shabiki atavyouchukulia mstari huo ni sawa kama mtu ataenjoy kuuskia kama "dancing with Moly" ni sawa na kwa wale wanaompenda Miley wakijiskia kama "dancing with Miley" ni sawa. Producer huyo amesema Miley kwa sasa anafanya kazi kwa nguvu zake zote kwaajili ya kutengeneza album yake mpya.

(NEWS) RAPPER WA MMG AZUNGUMZIA KUHUSU KUACHA MADAWA YA KULEVYA

    Gunplay amefunguka na kusema hivi sasa anajisikia vizuri baada ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kusema kwa sasa anadhani ndio utakua muda mzuri kwa yeye kufanya muziki mzuri.
   Rapper huyo anaetokea MMG amesema anawashauri wasanii wengine waache kutumia madawa ya kulevya kwani yatawaletea matatizo makubwa, akifunguka alisema alikua anapata tabu sana katika kuacha madawa japokuwa alikuwa akijisikia vibaya na pua yake kumuuma alikua akiendelea kuyatumia.
  Gunplay anajiandaa kwaajili ya kushiriki katika album ya group inayokwenda kwa jina la Self Made Vol 3.

Sunday 9 June 2013

(NEWS) MASHABIKI WAMLALAMIKIA OMARION KWA KUTOKUA NA ULINZI WA KUTOSHA

    Mashabiki waliohudhuria show ya Omarion wamekasirishwa kwa kitendo cha kutokuwepo kwa usalama wa kutosha katika show ya mkali huyu wa R&B iliyofanyika katika ukumbi wa Ole bar & Grill maeneo ya New York City.
    Wakiwa na hasira na jazba wengi wamesema wamekasirishwa kwa vurugu zilizotokea na kusababisha wengine kuumia huku wakisema awali kabla ya show waliambiwa kutakua na ulinzi wa  kutosha. Akizungumzia msala huo Omarion alisema kosa halikua lake bali ni la watu walioandaa show hiyo kwasababu hawakuweka ulinzi wa kutosha pia akasema kwa wale mashabiki walioumia kutokana na vurungu hizo kama wanataka kulipwa inabidi wakaangalie sehemu nyingine ila yeye hawezi kuwalipa.
  Omarion kwa sasa yupo chini ya Mybach Music Group (MMG) na anajiandaa kutengeneza project mpya.

(NEWS) BIG SEAN AELEZEA FURAHA YAKE BAADA YA KUFANYA KAZI NA EMINEM

     Sean Michael Anderson unaweza muita Big Sean asema amefurahi sana kufanya collabo na Eminem pia kupata nafasi ya kuongea nae. Big Sean amesema kabla ya kuingia studio kutengeneza kazi na Eminem walipata nafasi ya kupiga story.
    Big Sean anasema kila story aliyokua akimuhadithia Eminem kuhusiana na hustling za kimziki pamoja na kuperfom sehemu mbalimbali zilikua zinamshangaza Eminem kwani, hata yeye alipitia mishemishe hizo kipindi anatoka kimziki na hivo kujikuta wakiwa na mambo mengi yanayofanana.
   Marapper hawa wote wanatokea mji wa Detroit pande za United States na collabo yao inasubiriwa kwa hamu na wadau wa muziki.

Saturday 8 June 2013

(NEWS) MMG WAMUHITAJI MKALI JADAKISS

  Baada ya kufanya collabo na Rick Ross kwenye nyimbo ya "Oil Money Gang" ngoma ambayo itapatikana kwenye album ya Self made Vol 3 kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Jadakiss amesaini label na MMG.
  Akizungumzia kuhusu tetesi hizo Jada hakukubali wala kukataa kuwa atasaini na MMG japokua ana mkataba na Def Jam, MMG imeonyesha kutaka kuingia mkataba na wasani watatu ambao ni Jadakiss, Sheek Louch na Styles P.
  Jadakiss kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Big boy dialogue aliyomshirikisha The-Dream.
 

Friday 7 June 2013

(AUDIO) Nelly ft Future - Give U Dat

(AUDIO) Chris Brown ft Mario & Nicki Minaj - Somebody Else (Remix)

(AUDIO) Chamillionaire-Slow Loud & Bangin



(NEWS) TURK AFUNGUKA NA KUSEMA HAMJUI LIL WAYNE

   Turk amefunguka na kusema kuwa yeye hamfahamu Lil wayne wa sasa na kuwa anamjua zaidi lil wayne wa kipindi cha miaka ya nyuma.
   Turk ambaye alikuwa akiunda kundi moja na Lil wayne lilokuwa linakwenda kwa jina la Hot Boyz amesema tangu apate msala wa kukaa gerezani kwa kipindi cha miaka tisa kuna mambo mengi yamebadilika na kusema kama isingekuwa swala la kukaa gerezani angekuwa katika level ambayo anayo Lil wayne sasa kimziki.
  Turk amesema kuwa hivi sasa yupo katika movement ambazo zitamrudisha katika game ya muziki. Pia aliweza kuongelea swala linalomkabili Lil wayne la madawa ya kulevya na kusema hata yeye kipindi alivyokuwa na umri wa miaka 16 mpaka 17 alikua katika hali kama hiyo na alikuwa hamsikilizi mtu.

(NEWS) JE KUNA UWEZEKANO WA KUWEPO SEASON 3 YA WAWILI HAWA?

    Inawezekana wakawa wanatengeneza kitu ambacho ni special lakini wao hawakijui kwani kila kukicha kumekuwa na story mpya kati ya Chris Brown na mpenzi wake walie achana wiki chache zilizopita.
   Baada ya kuona tweets za kila mmoja akitumia muda kumlaumu mwenzie kwa kutengana kwao, sasa shughuli imehamia kwenye nyimbo. Chris ameachia nyimbo inayokwenda kwa jina la "somebody else" ambayo ukiisikiliza mashairi yake yanaonekana kulenga kabisa mahusiano yaliyovunjika kati yake na Rihanna.
  Kama haitoshi Rihanna nae amejibu mapigo kwenye nyimbo mpya ya Wale inayokwenda kwa jina la Bad(Remix) kwa kuimba chorus(kiitikio) kinachoonekana kujibu ngoma ya Chris Brown.
   Je kuna uwezekano kukawepo na season 3 ya watu hawa wawili?

(NEWS) MR NICE AHARIBU KENYA ATEMWA NA GRANDPA RECORDS

     Waswahili husema lisemwalo lipo kama halipo la jongea ndicho kilichotokea kwa Nice Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice, kulikua na story nyingi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mr Nice ametemwa na kampuni ya Grandpa na producer na owner wa Grandpa records anaejulikana kwa jina la Rafiga amedhibitisha na kusema kuwa wameamua kutemana na Mr Nice.
   Owner huyo amesema wameshindwa kwenda sawa na Nice kwasababu alikua na mikataba mingine nje ya grandpa na wao wanaheshimu sheria na wakaamua ni bora kutemana nae. Lakini kwa story zilizoenea kitaani zinasema Mr Nice katemwa kutokana na kuwa mlevi, mgovi, na mpenda wanawake hivo kusahau majukumu yaliyompeleka Kenya.
   Inasemekana kuwa mshkaji amekosa zaidi ya shilingi milioni 140 kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo, siku zote waswahili husema ukibebwa bebeka lakini ndugu yetu ameshindwa kubebeka


Thursday 6 June 2013

(NEWS) MTU TATU NDANI YA TRACK MOJA JUSTIN TIMBERLAKE, JAY Z NA NAS

   Baada ya kufanya kazi moja matata sana ambayo ilimrudisha upya katika game ya muziki JustinTimberlake ambayo alipigwa tafu na mkali Jay Z sasa wajipanga tena.
   Justin alionekana akiwa na Jay Z pamoja na mkongwe mwingine kwenye game ya Hip Hop Nas Escobar wakiwa wanajiaanda kutengeneza nyimbo mpya ya pamoja na mzigo mzima wa kutengeneza ngoma hiyo utafanywa producer Timbaland.
   Kama haitoshi siku za karibuni alionekana pia akiwa na Pharrell Wlliams wakijiandaa kutengeneza track. Kwa wale wanaoelewa shughuli ya Nas na Jay Z  ambayo ikijumuishwa na Justin watakua wanafahamu nini kitakacho kuja.

(AUDIO) Kid Ink ft Sterling Simms-Was It Worth It

(AUDIO) Massari-The Money (All She Want)

(AUDIO) Akon-Breakdown


(NEWS) WAKAZI WA MOROGORO WAPATA NAFASI YA KUUAGA MWILI WA NGWAIR

   Leo wakazi wa mji wa Morogoro walipata nafasi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya Albert Mangwea ambae alifariki wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini.
  Shughuli nzima ilifanyikia katika uwanja wa Jamhuri na kisha mwili wa marehemu ukapelekwa nyumbani kwao Kihonda kwa ajili ya mazishi. Mungu aulaze mwili wa marehemu mahala pema peponi