Thursday 13 June 2013

(NEWS) MWEZI MBAYA KWA 2 CHAINZ(Tity Boi)

  Ukiwa sio mwezi mzuri kwa rapper 2 Chainz kutokana na kukumbwa na misala kila kukicha. Baada ya jana kuonekana akiwa amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Los Angels International Airport kutokana na kutuhumiwa kukutwa na bangi leo kimenuka tena.
  Akiwa maeneo ya San Fransico mkali huyu alivamiwa na wakabaji(waporaji) ambapo pia ilisikika milio ya risasi pande hizo. Inasemekana 2 Chainz alikuwa na wapambe wake lakini baada ya kusikia milio ya risasi walijikuta wa kihangaika kukimbia huku na kule kama mende. Wakabaji hao walifanikiwa kuondoka na pochi ya rapper huyo, lakini lakumshukuru Mungu rapper huyo hakuweza kujeruhiwa na risasi pia 2 Chainz alikataa kuzungumza na police kwa kusema atashughulikia tatizo mwenyewe.

No comments:

Post a Comment