Monday 10 June 2013

(AUDIO) Ciara-Boy Outta Here


(NEWS) UTATA WA MASHAIRI ULIOPO KATIKA NYIMBO YA MILEY WAWACHANGANYA MASHABIKI

   Utata wa mashairi uliopo katika single mpya "We can't stop" ya mwanadada Miley umewafanya mashabiki wake kujiuliza  kuumiza vichwa sana kwani wameshindwa kuelewa msanii huyu ameimba nini.
  Ngoma hiyo ambayo itapatikana katika album mpya ya Miley ambayo inategemewa kutoka mwaka, mashabiki wengi wanashindwa kuelewa kuwa kwenye ngoma hiyo mwanadada ameimba "dancing with Molly" au ni "dancing with Miley".
  Akizungumzia kuhusiana na ishu hiyo producer alietengeneza ngoma hiyo Mike Will Made It amesema kuwa vyovyote shabiki atavyouchukulia mstari huo ni sawa kama mtu ataenjoy kuuskia kama "dancing with Moly" ni sawa na kwa wale wanaompenda Miley wakijiskia kama "dancing with Miley" ni sawa. Producer huyo amesema Miley kwa sasa anafanya kazi kwa nguvu zake zote kwaajili ya kutengeneza album yake mpya.

(NEWS) RAPPER WA MMG AZUNGUMZIA KUHUSU KUACHA MADAWA YA KULEVYA

    Gunplay amefunguka na kusema hivi sasa anajisikia vizuri baada ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kusema kwa sasa anadhani ndio utakua muda mzuri kwa yeye kufanya muziki mzuri.
   Rapper huyo anaetokea MMG amesema anawashauri wasanii wengine waache kutumia madawa ya kulevya kwani yatawaletea matatizo makubwa, akifunguka alisema alikua anapata tabu sana katika kuacha madawa japokuwa alikuwa akijisikia vibaya na pua yake kumuuma alikua akiendelea kuyatumia.
  Gunplay anajiandaa kwaajili ya kushiriki katika album ya group inayokwenda kwa jina la Self Made Vol 3.