Monday 10 June 2013

(NEWS) RAPPER WA MMG AZUNGUMZIA KUHUSU KUACHA MADAWA YA KULEVYA

    Gunplay amefunguka na kusema hivi sasa anajisikia vizuri baada ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kusema kwa sasa anadhani ndio utakua muda mzuri kwa yeye kufanya muziki mzuri.
   Rapper huyo anaetokea MMG amesema anawashauri wasanii wengine waache kutumia madawa ya kulevya kwani yatawaletea matatizo makubwa, akifunguka alisema alikua anapata tabu sana katika kuacha madawa japokuwa alikuwa akijisikia vibaya na pua yake kumuuma alikua akiendelea kuyatumia.
  Gunplay anajiandaa kwaajili ya kushiriki katika album ya group inayokwenda kwa jina la Self Made Vol 3.

No comments:

Post a Comment