Wednesday 26 March 2014

YG APIGA BAO KWENYE MAUZO YA WEEK YA KWANZA YA ALBUM YAKE YA "MY KRAZY LIFE"

Rapper YG anaetokea pande za west coast pande za US ameendelea kufanya vizuri baada ya kuachia album yake inayokwenda kwa jina la "My Krazy Life" last week na mauzo ya week ya kwanza yametoka na amefanikiwa kuuza copy 59,703 kwa week yake ya kwanza ni moja kati ya rappers wadogo akiwa amezaliwa mwaka 1990 lakini anafanya vizuri tunasubiria tuone je ataweza kuendelea kuuza nakala ngapi kwa album yake hii.

REMY MA AELEZEA MIPANGO YAKE YA KURUDI KWENYE GAME LA MUZIKI

Yule mwanadada ambaye alikua akisukuma game la muziki vilivyo na kusababisha watu wengi kumuita rapper bora wa kike sasa anatarajia kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 6,Huyu si mwingine bali ni Remy Ma ambaye alikua first lady wa kundi la Terror squad lilokua likiongozwa na Fat Joe, akizungumzia kuhusu kurejea kwenye game Remy alianza kwa kusema kuwa amemaliza beef lake na Fat Joe na kuwa walipata muda wa kuongea kwa simu na kuyaweka sawa, Remy ambaye ni mke wa rapper Papoose amesema amepokea ofa za kufanya reality shows kibao kasema anajipanga kurudi kwenye game na kusema anawakubali rappers wengi mmoja wao akiwa Meek Mill.