Wednesday 26 March 2014

REMY MA AELEZEA MIPANGO YAKE YA KURUDI KWENYE GAME LA MUZIKI

Yule mwanadada ambaye alikua akisukuma game la muziki vilivyo na kusababisha watu wengi kumuita rapper bora wa kike sasa anatarajia kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 6,Huyu si mwingine bali ni Remy Ma ambaye alikua first lady wa kundi la Terror squad lilokua likiongozwa na Fat Joe, akizungumzia kuhusu kurejea kwenye game Remy alianza kwa kusema kuwa amemaliza beef lake na Fat Joe na kuwa walipata muda wa kuongea kwa simu na kuyaweka sawa, Remy ambaye ni mke wa rapper Papoose amesema amepokea ofa za kufanya reality shows kibao kasema anajipanga kurudi kwenye game na kusema anawakubali rappers wengi mmoja wao akiwa Meek Mill.

No comments:

Post a Comment