Monday 17 June 2013

(NEWS) DRAKE ATANGAZA KUFANYA TOUR KATIKA MAJIJI 41

     Drake atangaza tour kwa ajili ya maandalizi ya kupush album yake itakayokwenda kwa jina la Nothing was the same.
    Tour hiyo itafanyika maeneo ya Amerika ya kaskazini na atakuwa na wasanii ambao watampiga tafu katika tour hiyo ambao ni Future na Miguel. Tour hiyo itapita kwenye majiji 41 na itaanza September 25

(NEWS) ALBUM YA KANYE WEST YAVUJA MTANDAONI

      Yakiwa yamebakia masaa kadhaa album ya Kanye West kuachiwa rasmi limeibuka balaa lingine ambalo lime mchanganya Yeezy.
      Habari zinasema kuwa album hiyo inayokwenda kwa jina la Yeezus imevuja siku ya ijumaa na wataalamu wanasema ishu hiyo imemchanganya Kanye ambaye hivi sasa ni baba wa mtoto mmoja. Kampuni ya Kanye imeshaanza kushughulikia wahusika wanao husika na kuvujisha album hiyo na wamesema watawachukulia hatua za kisheria kwani wamevuruga biashara.
    Kumekua na tabia ya uvujishaji wa album za masuper star sana na taarifa zinasema kuwa watu wa karibu na ma-star ndio wamekuwa wakihusika zaidi 

(NEWS) JAY Z ATANGAZA ALBUM MPYA NA SIKU YA KUTOKA

    Akiwa ameshaingia kwenye dili na kampuni ya Samsung  Jay Z ametaja jina la album na tarehe ambayo album hiyo itatoka.
   Jay Z alifunguka na kusema kuwa album itakwenda kwa jina la "Magna Carta Holy Grail" itakuwa available kuanzia July 4 kwa wateja milioni moja wa Samsung ambao watakua wanatumia application maalumu kwaajili ya kuipata album hiyo na kwa watumiaji wengine itakuwa available baada ya masaa 72 baada ya kuachiwa  July 4 na tayari kampuni ya Samsung imeshanunua nakala zaidi ya milioni za album hiyo ya Jay Z.