Sunday 9 June 2013

(NEWS) MASHABIKI WAMLALAMIKIA OMARION KWA KUTOKUA NA ULINZI WA KUTOSHA

    Mashabiki waliohudhuria show ya Omarion wamekasirishwa kwa kitendo cha kutokuwepo kwa usalama wa kutosha katika show ya mkali huyu wa R&B iliyofanyika katika ukumbi wa Ole bar & Grill maeneo ya New York City.
    Wakiwa na hasira na jazba wengi wamesema wamekasirishwa kwa vurugu zilizotokea na kusababisha wengine kuumia huku wakisema awali kabla ya show waliambiwa kutakua na ulinzi wa  kutosha. Akizungumzia msala huo Omarion alisema kosa halikua lake bali ni la watu walioandaa show hiyo kwasababu hawakuweka ulinzi wa kutosha pia akasema kwa wale mashabiki walioumia kutokana na vurungu hizo kama wanataka kulipwa inabidi wakaangalie sehemu nyingine ila yeye hawezi kuwalipa.
  Omarion kwa sasa yupo chini ya Mybach Music Group (MMG) na anajiandaa kutengeneza project mpya.

(NEWS) BIG SEAN AELEZEA FURAHA YAKE BAADA YA KUFANYA KAZI NA EMINEM

     Sean Michael Anderson unaweza muita Big Sean asema amefurahi sana kufanya collabo na Eminem pia kupata nafasi ya kuongea nae. Big Sean amesema kabla ya kuingia studio kutengeneza kazi na Eminem walipata nafasi ya kupiga story.
    Big Sean anasema kila story aliyokua akimuhadithia Eminem kuhusiana na hustling za kimziki pamoja na kuperfom sehemu mbalimbali zilikua zinamshangaza Eminem kwani, hata yeye alipitia mishemishe hizo kipindi anatoka kimziki na hivo kujikuta wakiwa na mambo mengi yanayofanana.
   Marapper hawa wote wanatokea mji wa Detroit pande za United States na collabo yao inasubiriwa kwa hamu na wadau wa muziki.