Friday 4 April 2014

JAY Z AMFOLLOW JOE BUDDEN TWITTER

Katika hali ya kushangaza kidogo mtu mzima Jay Z ameonekana kumfollow rapper Joe Budden kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Jay ambaye si mtumiaji mkubwa sana wa mtandao huo amewashangaza wengi kwani hana tabia ya kufollow wasanii wala watu maarufu kwani hata Beyonce ambaye ni mkewe hajamfollow.Kipindi cha nyuma Jay Z alishawahi kuwa na beef na Joe budden na haijajulikana ni nini kinachoendelea au kipi kitafuata baada ya tukio hilo.

SCARFACE KUACHIA ALBUM ITAKAYOKWENDA KWA JINA LA DEEPLY ROOTED

Legendary Scarface ajipanga kuachia album baada ya kukaa kitambo bila kuajia album, mkali huyu kutokea pande za Houston huko Marekani amesema album itakwenda kwa jina la "Deeply Rooted" pia nje ya album Scarface anatengeneza kitabu chake kinachokwenda kwa jina la Deeply Rooted ambacho kinaandikwa na mwandishi Benjamin Meadows amesema kitabu hicho kitakua kinaongelea maisha yake kwa ujumla,mambo mazuri,mabaya na haraki za game la muziki.