Thursday 13 June 2013

(NEWS) MWEZI MBAYA KWA 2 CHAINZ(Tity Boi)

  Ukiwa sio mwezi mzuri kwa rapper 2 Chainz kutokana na kukumbwa na misala kila kukicha. Baada ya jana kuonekana akiwa amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Los Angels International Airport kutokana na kutuhumiwa kukutwa na bangi leo kimenuka tena.
  Akiwa maeneo ya San Fransico mkali huyu alivamiwa na wakabaji(waporaji) ambapo pia ilisikika milio ya risasi pande hizo. Inasemekana 2 Chainz alikuwa na wapambe wake lakini baada ya kusikia milio ya risasi walijikuta wa kihangaika kukimbia huku na kule kama mende. Wakabaji hao walifanikiwa kuondoka na pochi ya rapper huyo, lakini lakumshukuru Mungu rapper huyo hakuweza kujeruhiwa na risasi pia 2 Chainz alikataa kuzungumza na police kwa kusema atashughulikia tatizo mwenyewe.

(NEWS) LANGA AFARIKI DUNIA LEO SAA KUMI JIONI

  Msanii aliyekuwa akiwakilisha vizuri muziki wa BongoFleva kwa upande wa Hip Hop anaefahamika kwa jina la Langa Kileo amefariki leo jioni.
  Akidhibitisha taarifa hizo baba mzazi wa msanii huyu, anasema Langa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
  Taratibu za msiba zinaendelea nyumbani kwao Mikocheni na mama mzazi wa msanii anatarajiwa kufika nchini kesho akitokea nchini Marekani.
  Mungu ailaze roho ya marehemu Langa mahala pema peponi.