Sunday 9 June 2013

(NEWS) MASHABIKI WAMLALAMIKIA OMARION KWA KUTOKUA NA ULINZI WA KUTOSHA

    Mashabiki waliohudhuria show ya Omarion wamekasirishwa kwa kitendo cha kutokuwepo kwa usalama wa kutosha katika show ya mkali huyu wa R&B iliyofanyika katika ukumbi wa Ole bar & Grill maeneo ya New York City.
    Wakiwa na hasira na jazba wengi wamesema wamekasirishwa kwa vurugu zilizotokea na kusababisha wengine kuumia huku wakisema awali kabla ya show waliambiwa kutakua na ulinzi wa  kutosha. Akizungumzia msala huo Omarion alisema kosa halikua lake bali ni la watu walioandaa show hiyo kwasababu hawakuweka ulinzi wa kutosha pia akasema kwa wale mashabiki walioumia kutokana na vurungu hizo kama wanataka kulipwa inabidi wakaangalie sehemu nyingine ila yeye hawezi kuwalipa.
  Omarion kwa sasa yupo chini ya Mybach Music Group (MMG) na anajiandaa kutengeneza project mpya.

No comments:

Post a Comment