Friday 7 June 2013

(NEWS) TURK AFUNGUKA NA KUSEMA HAMJUI LIL WAYNE

   Turk amefunguka na kusema kuwa yeye hamfahamu Lil wayne wa sasa na kuwa anamjua zaidi lil wayne wa kipindi cha miaka ya nyuma.
   Turk ambaye alikuwa akiunda kundi moja na Lil wayne lilokuwa linakwenda kwa jina la Hot Boyz amesema tangu apate msala wa kukaa gerezani kwa kipindi cha miaka tisa kuna mambo mengi yamebadilika na kusema kama isingekuwa swala la kukaa gerezani angekuwa katika level ambayo anayo Lil wayne sasa kimziki.
  Turk amesema kuwa hivi sasa yupo katika movement ambazo zitamrudisha katika game ya muziki. Pia aliweza kuongelea swala linalomkabili Lil wayne la madawa ya kulevya na kusema hata yeye kipindi alivyokuwa na umri wa miaka 16 mpaka 17 alikua katika hali kama hiyo na alikuwa hamsikilizi mtu.

No comments:

Post a Comment