Friday 7 June 2013

(NEWS) MR NICE AHARIBU KENYA ATEMWA NA GRANDPA RECORDS

     Waswahili husema lisemwalo lipo kama halipo la jongea ndicho kilichotokea kwa Nice Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice, kulikua na story nyingi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mr Nice ametemwa na kampuni ya Grandpa na producer na owner wa Grandpa records anaejulikana kwa jina la Rafiga amedhibitisha na kusema kuwa wameamua kutemana na Mr Nice.
   Owner huyo amesema wameshindwa kwenda sawa na Nice kwasababu alikua na mikataba mingine nje ya grandpa na wao wanaheshimu sheria na wakaamua ni bora kutemana nae. Lakini kwa story zilizoenea kitaani zinasema Mr Nice katemwa kutokana na kuwa mlevi, mgovi, na mpenda wanawake hivo kusahau majukumu yaliyompeleka Kenya.
   Inasemekana kuwa mshkaji amekosa zaidi ya shilingi milioni 140 kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo, siku zote waswahili husema ukibebwa bebeka lakini ndugu yetu ameshindwa kubebeka


No comments:

Post a Comment