Friday 7 June 2013

(NEWS) JE KUNA UWEZEKANO WA KUWEPO SEASON 3 YA WAWILI HAWA?

    Inawezekana wakawa wanatengeneza kitu ambacho ni special lakini wao hawakijui kwani kila kukicha kumekuwa na story mpya kati ya Chris Brown na mpenzi wake walie achana wiki chache zilizopita.
   Baada ya kuona tweets za kila mmoja akitumia muda kumlaumu mwenzie kwa kutengana kwao, sasa shughuli imehamia kwenye nyimbo. Chris ameachia nyimbo inayokwenda kwa jina la "somebody else" ambayo ukiisikiliza mashairi yake yanaonekana kulenga kabisa mahusiano yaliyovunjika kati yake na Rihanna.
  Kama haitoshi Rihanna nae amejibu mapigo kwenye nyimbo mpya ya Wale inayokwenda kwa jina la Bad(Remix) kwa kuimba chorus(kiitikio) kinachoonekana kujibu ngoma ya Chris Brown.
   Je kuna uwezekano kukawepo na season 3 ya watu hawa wawili?

No comments:

Post a Comment