Friday 30 May 2014

NICKI MINAJ AINGIZA PESA KWA KUONEKANA KWENYE BIRTHDAY PARTY

Nicki Minaj ni moja kati ya mastar ambao wanaweza kuacha kufanya muziki na bado akawa anapiga hela ndefu kupitia sura yake tu. Hili limejidhiirisha hivi karibuni baada ya bondia Floyd Mayweather kumlipa kiasi cha dola 50,000 kwajili ya kuhudhuria tu kwenye birthday party ya mtoto wake wa kike anayefahamika kwa jina la Iyanna. Inasemekana kiasi hicho cha pesa ni sawa na mshara wa mwalimu wa kawaida wa Marekani ambao analipwa kwa mwaka. Birthday party ya mwaka jana ya Iyanna iliudhuriwa na Justin Beiber. Nick kwa sasa ameachia single yake mpya inayokwenda kwa jina la "Pills N Potions," ikiwa ni maandalizi ya album yake itakayokwenda kwa jina la The Pinkprint.

No comments:

Post a Comment